Offline
Menu
MAOMBI JUU YA KAZI/UCHUMI/BIASHARA
By CRISPIN ADAM
Published on 09/27/2025 10:42
News

MAOMBI JUU YA KAZI/UCHUMI/BIASHARA

 

OMBI KUU: KUOMBEA KAZI ZA MIKONO YAKO.

 

(1) OMBEA MSINGI WA KAZI YAKO.

 

Zaburi 11:3

" Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?"

Marko 12:10

" Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni."

YESU NDIYE JIWE KUU LA PEMBENI.

Lazima ujue MSINGI WA KAZI ZAKO, LAZIMA YESU AWE KAMA JIWE KUU LA PEMBENI, MSINGI WA KIBIASHARA KAMA HAUNA YESU NI HATARI SANA .

Ngoja nikuonyeshe kitu hapa.

Luka 5:4-6 (KJV) "Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;" 

HUYU MFANYABIASHARA ALIKUWA KAVUA USIKU KUCHA NA HAKUPATA KITU KABISA ,YESU ALIPOKUJA AKAMWAMBIA AWEKE NYAVU ZAKE MPAKA KILINDINI,JE UNAJUA NI KWA NINI ALIMWAMBIA AWEKE MPAKA KILINDINI?

Zaburi 24:1-2 (KJV) " Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.

Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha."

Kilindini ndipo penye misingi ya biashara waliyoifanya hawa ndugu ,Sasa hawakujua kuna UHUSIANO WA NENO LA KRISTO NA ENEO LAO LA KAZI AU NA WALICHOKIFA.

HAPO MWANZO KULIKUWEPO NENO ,NENO NDIYE MWANZO ,MWANZO NI MSINGI NA YESU NDIYE JIWE KUU LA PEMBENI KWENYE MSINGI.

WALITWEKA NYAVU ZAO MAHALI AMBAPO HAPANA MSINGI,YESU AKAONA AKAWAAMBIA SOGEENI HADI KILINDINI WEKENI NYAVU ,KWA NENO LAKE WALIPOWEKA WAKAJA NA SAMAKI WAKUTOSHA.

 

MAOMBI

* Baba katika Jina la Yesu

* Ninaomba rehema juu ya misingi na mwanzo wa kazi zangu,pale ambapo sikukushirikisha

* Ninaomba unisamehe ,unitakase na kunirehemu kwa damu yako eeh Yesu.

* Ninakukaribisha kwenye mwanzo wa kazi za mikono yanu,uwe Mungu,uwe  kiongozi na muasisi wa kazi zangu ,kwa jina la Yesu.

 

( 2)OMBA WATU SAHIHI na (Wateja) Juu ya kazi yako.

 

Isaya 43:4 (KJV) "Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako."

Isaya 61:5 (KJV) "Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu."

 

MAOMBI:

* Baba katika jina la Yesu

* Ninaomba  neema zako kwenye kazi yangu

* Eeh Mungu ninaomba uniinulie watu sahihi kwenye kazi zangu

* Bwana Yesu ,ninaomba unikutanishe na watu sahihi kwenye kazi zangu

* Bwana Yesu ninaomba wateja kwenye kazi zangu na biashara yangu

* Bwana Yesu  ninaomba  watu wa kila lugha,kila kabila  na waje kwenye kazi za mikono yangu

* Mungu ninaomba neema ya kukutana na watu watakaonisogeza mahali pa  juu zaidi kibiashara ,katika Jina la Yesu.

 

( 3 ) Omba roho ya Ubunifu kwenye kazi zako .

 

Kutoka 31:1-6 (KJV) "Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;

nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,

ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,

na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza;"

 

MAOMBI 

* Baba katika jina la Yesu,ninaomba ile roho ya Ubunifu na iwe kwenye maisha yangu

* Ninaomba neema ya kufanya kazi zangu kwa ubunifu wa hali ya juu 

* Ninaomba uniumbie roho ya ubunifu ndani yangu kwa jina la Yesu

 

( 4 )Kataa roho ya Uharibifu na mauti kwenye kazi zako.

 

Wimbo Ulio Bora 2:15

"Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua."

Malaki 3:11 (KJV) "Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi."

MAOMBI

* Baba katika Jina la Yesu

* Ninakataa kila roho ya mauti kwenye kazi za mikono yangu

* Ninakataa kila roho ya kufilisika kwa jina la Yesu

* Ninakataa kila roho ya kuibiwa kwenye maisha yangu

* Ninakataa kila roho ya kurudishwa nyuma kwa jina la Yesu

* Nikataa kutapeliwa,ninakataa kudhulumiwa ,ninakataa mali zangu kuharibika kwa jina la Yesu 

 

( 5 )Omba Mungu akupe kibali kwa unaofanyanao kazi au biashara.

 

1 Samweli 2:26

Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa Bwana, na kwa watu pia.

Zaburi 19:14

Maneno ya kinywa changu, Na mawazo(WAZO LA KIBIASHARA) ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.

Zaburi 106:4

Ee Bwana, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako,

Mithali 3:4

Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

 

MAOMBI

* Baba katika Jina la Yesu

* Ninaomba roho ya kibali juu yangu na juu ya kazi za mikono yangu

* Kibali chako kiwe kwenye biashara zangu na kazi zangu kwa jina  la Yesu

* Kila mikono yangu itakachokifanya ,kiwe na kibali kwa jina la Yesu

* Ninaomba neema yako ishikamane na kazi zangu na kuweka kibali kikubwa kwa kila mtu kwa jina la Yesu.Amen

 

(6) Omba Mungu aachilie baraka zake kazini kwako.

 

Kumbukumbu la Torati 16:15

"Siku saba mfanyie sikukuu Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua Bwana; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, atakubarikia katika maongeo yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa."

 

MAOMBI

 

* Bwana unibariki mimi na kazi zangu

* Unibariki mimi na uzao wangu

* Unibariki mimi na ninaofanya nao kazi zangu 

* Uubariki mtaji wangu,ukazae sana

* Uwabariki na wote walio na nia njema na kazi zangu  kwa jina la Yesu.

 

“Karibu sana kwenye huduma yetu ya  maombi na kujifunza neno la Mungu hapa KWA ZOO,BUYUNI- CHANIKA,ni Sehemu nzuri ya Maombi/Maombezi/Neno halisi la Mungu/ushauri, UKUE KIROHO huduma zetu ni Bure kabisa,wasiliana na sisi kwa No. 0754566405/06821949191”  KARIBU SANA

Comments
Comment sent successfully!