

MWONGOZO WA MAOMBI JUU YA MISINGI YA NDOA .
OMBI KUU: BOMOA MADHABAHU ZA GIZA ZINAZOFUATILIA NDOA YAKO ILI KUHARIBU NA KUBOMOA .
Mungu anakaa kwenye madhabahu na shetani naye anakaa kwenye madhabahu,Kwenye madhababu kuna roho ambazo huwa zinaitumikia madhababu ,ni roho zilizo wahudumu wa madhabahu hizo,Na kwenye madhababu ndipo zinapokaa roho za watu pia.
Maisha ya mwanadamu kama hayapo kwenye madhababu ya Mungu basi yapo kwenye madhababu ya Shetani na Hiki ndicho kilichomleta Yesu ,KUJA KUMKOMBOA MWANADAMU KUTOKA HUKO KWENYE MADHABAHU ZA GIZA.
Na Mungu ni Mwangalifu sana ,UKIWA NI MTU WAKE CHA KWANZA UKIWA UNATEMBEA NAYE ,ANASEMA NA WEWE KWANZA NA KUKUPA TAADHARI JUU YA MADHABAHU ZA MIUNGU MINGINE KUWA USIFANYE NAO MAAGANO.
Kutoka 23:32 (KJV) " Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao."
Kutoka 34:13
" Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao."
MAAGANO NI KITU CHA KIMADHABAHU.
NDIYO SABABU PIA NDOA INAFUNGWA MADHABAHUNI.
KWENYE HIYO MADHABABU NDOA INAPOFUNGWA KUNA MUNGU AU SHETANI.
KILA MADHABAHU INA MUNGU WAKE.
NDIYO SABABU KUNA MADHABAHU ZA AINA MBILI KUU
1.MADHABAHU TAKATIFU YA MUNGU ALIYE HAI
2.MADHABABU YA MASHETANI.
Kwenye madhabahu Yeyote IMEBEBA MFUMO WA MAISHA WA WATU WALIOAMUA KUMFUATA MUNGU WA HIYO MADHABAHU.
MADHABAHU IMEBEBA ( ROHO ZA WATU/MAAGANO/ROHO/ MANENO/SAUTI/MUNGU AU MIUNGU/SADAKA N.K) KWA KIFUPI NI KUWA MADHABABU INATOA MFUMO WA MAISHA ( LIFE STAILY) KWA WATU WA ENEO HUSIKA WANAOISHI KWENYE ENEO HUSIKA AU FAMILIA HUSIKA ,MAANA ULIANZA KUONGELEA JUU YA MADHABAHU ZIPO ZA KIFAMILIA/KIMTAA/KIMKOA/KIKANDA/KITAIFA/KIMATAIFA .NK
SASA KUNA WATU AMBAO MADHABAHU ZINAWEZA KUWAKATALIA KWA HABARI YA KUWA NA NDOA AU KUNA WATU AMBAO MADHABAHU ZAKO ZINAWEZA KUWASHIKILIA NA ZISIWAACHIE KABISA HATA WAKIOLEWA WANAENDA KWENYE NDOA NA MADHABAHU ZAO NA MIUNGU YAO,HAPO NDIYO INAKUWA KAZI KWELI KWELI.
MFANO: 1
YAKOBO ALIPOMCHUKUA LEA NA RAHELI KAMA WAKE ZAKE ,WAKE ZAKE HAWA HAWAKUIACHA MIUNGU YA BABA YAO ,WALIKUJA NAYO KWENYE MAISHA MAPYA YA NDOA YA NDUGU YETU YAKOBO,YAKOBO AKAWA ANAFUATILIWA SANA NA LABANI NA VITA VIKAWA VIKUMBWA ,HAKUJUA KUWA HUKO ALIPOOA WALE MABINTI WANAABUDU MIUNGU NA YAKOBO HAJUI.
Mwanzo 31:30
" Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu?"
Mwanzo 35:2
"Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu."
Mwanzo 35:4
" Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu."
Yakobo alioa Familia ambayo MABINTI WALIONDOKA NA MIUNGU YA BABA YAO NA KWENDA KUANZA FAMILIA MPYA ,MAANA YAKE MISINGI YA FAMILIA HII ILIKUWA MIBOVU KABISA.
●Wewe haujawahi kuona mtu anaolewa lakini ANAINGIA KWENYE NDOA NA MATAMBIKO KIBAO NA KAFARA KIBAO KAFANYIWA ILI AKADUMU KWENYE NDOA,USHIRIKINA UMEFANYWA HASWA.
●WEWE HAUJAWAHI KUONA MTU ANAOLEWA ANAKUJA NA TARATIBU ZA KWAO ZA KIMILA KUJA KUMRUBUNI MWEZI WAKE NAYE AZIFUATE
●KUNA WATU WANAOA/KUOLEWA WANAKUJA NA ZANA ZA KISHIRIKINA HAUJAWAHI KUONA NAKUAMBIA,HATA NYUMBA WANAYOIISHI LAZIMA IZINDIKWE VILIVYO.
MFANO : 2
BINTI ALIYE OLEWA NA WANAUME SABA NA WOTE WAK
Madhabahu ya kwao HAWA VIJANA haikutana Huyu Binti awe na ndoa ,NA HII FAMILIA MADHABAHU YAKE ILIUA WATOTO WOTE SABA WA KIUME WALIO OA HUYU BINTI ,Watu wakamfuata Yesu wakamueleza habari za huyu binti.
Mathayo 22:25-27 (KJV) " Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.
Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.
Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye."
●Kila akioa mke anakufa
●Kila akiolewa anakufa
●Kila akiolewa anaachika ( Kuna familia za hivi ujue)
●Kila akiolewa ,ataolewa ila hazai watoto
●Kila akioa wanawake hawakai,kila siku anakuwa ni wa kuoa tu na kuacha
●Baada ya kuoa tu,AKAFILISIKA
●BAADA YA KUOA AKAFUKUZWA KAZI
●MWINGINE KAOA ILA KILA MAHALI ANA WANAWAKAE WA KUTOSHA AU WANAUME ( ukifuatilia kwao ndivyo walivyo)
●Wengine tangu waingie kwenye ndoa Hakuna wanachofanya wakafanikiwa
●
●Wengine hawaoi
●Wengine hawaolewi
KUNA MAMBO MENGI SANA KWENYE MAISHA YA WATU,WATU WANAPITIA MENGI ,NA WENGI HAWASEMI ILA WANATESEKA SANA KWENYE NDOA, WENGINE WANAFIKIRI "NI TABIA YA MTU" VINGINE SI TABIA NI UNAPAMBANA NA MADHABAHU ZA FAMILIA ZA WATU,UMEOA AU KUOLEWA KWENYE FAMILIA ULIYODHANI UNAIJUA KUMBE HUIJUI.....UNAFIKIRI UNAPAMBANA NA TABIA KUWA MWENZAKO KABADILIKA..SI KABADILIKA BALI MAISHA YAKE YAMEFUGWA KWENYE MADHABAHU ZA FAMILIA NA UKOO WAKE,NA ANAYETESEKA NI WEWE.
YAKOBO ALIPAMBA NA ALIKUJA KUJUA BAADAYE SANA KUWA ALIPOOA WANATEGEMEA MIUNGU KUFANIKISHA MAMBO YAO.
●MUONGOZO WA MAOMBI YA KUKATAA ROHO YA UHARIBIFU KWENYE FAMILIA YAKO
“Kama misingi ikiharibika,
Mwenye haki atafanya nini?” Zaburi 11:3
“Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.” Isaya 58:12
●MAOMBI
I. Baba katika jina la Yesu,asante kwa neema yako na baraka zako kwangu na familia yangu.
II. Nimesimama mbele zako eeh Yesu ,kuomba rehema na toba juu ya familia yangu.
●TOBA KWENYE MISINGI YA FAMILIA YA YAKO.
2 Nya 7:14 (SUV)
.... “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”
III. Ninaomba rehema zako kwenye misingi ya familia yangu eeh Yesu.
IV. Ikiwa kuna misingi mibovu ninayunyiza damu ya Yesu kwenye misingi ya familia yangu.
V. Ikiwa kuna maagano au matambiko yalifanyika na yakampa adui uhalali wa kuishambulia familia yangu,ninaomba rehema na toba mbele zako eeh Bwana.
VI. Ikiwa kwenye familia kuna mtu anaendelea kuabudu miungu au kuitegemea kwa siri ,ninaomba rehema juu yake eeh Yesu.
VII. Ninakataa kila roho za giza zinazoitawala familia yangu kwa jina la Yesu.
VIII. Ninanyunyiza damu ya Yesu juu ya kila nafsi ya mwanafamilia kwa jina la Yesu.
IX. Ninaondoa kila laana na matamko ya kipepo kwenye familia yangu kwa jina la Yesu.
●VUNJA KILA MADHABAHU YA GIZA KWENYE FAMILIA NA MISINGI YAKE
“Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi;
nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.” Kumbukumbu 12:2-3
X. Baba katika jina la Yesu,ninakata kila madhabahu ya giza kwenye familia yangu.
XI. Ninafunga kila nguvu za giza kwenye familia yangu ,kwa jina la Yesu.
XII. Ninafunga kila roho za giza zilizokuwa zinatumika kuharibu familia yangu kwa jina la Yesu.
XIII. Ninateketeza kila mipango ya siri ya uharibifu iliyotengenezwa na madhabahu za giza juu ya familia yangu kwa jina la Yesu.
XIV. Ninafuta kila kafara au sadaka za giza kwenye familia yangu ,Kwa damu ya Yesu.
XV. Ninatakasa ardhi na anga la familia yangu ,kwa jina la Yesu.
XVI. Ninafuta majina na kazi za wana familia kwenye madhabahu za giza kwa Jina la Yesu.
XVII. Ninaondoa kila muunganiko wa kipepo uliokuwepo kwa jina la Yesu.
XVIII. Ninangusha kila mfumo wa utendaji kazi wa giza na madhabahu hizo kwa jina la Yesu.
●ONDOA KILA MAUTI NA UHARIBUFU KWENYE FAMILIA YAKO
..... “mauti imemezwa kwa kushinda.” 1Wakoritho 15:54
XIX. Baba katika jina la Yesu ninaipinga mauti na uharibifu kwenye familia yangu ,kwa jina la Yesu
XX. Kila mauti iliyojificha kwa siri ,ninaing`oa kwa jina la Yesu.
XXI. Kila mpango wa kuzimu juu ya familia yangu,ninauondoa kwa jina la Yesu.
XXII. Kila uharibifu ninaupinga kwa jina la Yesu.
XXIII. Ninakataa magonjwa,wivu mbaya kwa jina la Yesu.
XXIV. Ninazipinga ajali na kila roho ya kupoteza au kuibiwa na maonevu ya kila namna kwa jina la Yesu.
XXV. Kila mateso na yakome kwa jina la Yesu.
XXVI. Roho ya hofu,woga naikataa kwenye familia kwa jina la Yesu.
XXVII. Kila roho ya vurugu na kukosa furaha ninaiondoa kwa jina la Yesu.
●TAMKA BARAKA KWENYE FAMILIA
Ebr 6:14 (SUV)
... “akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.”
XXVIII. Baba katika jina la Yesu,ninaomba ile roho ya baraka na iwe kwenye familia yangu.
XXIX. Ile nguvu ya uwezeshi na ije kwenye familia yangu kwa jina la Yesu.
XXX. Baraka kwenye afya,Uchumi,amani kwenye kila eneo kwa jina la Yesu.
XXXI. Ninatamka uponyaji ,kufunguliwa kwenye kila eneo kwa wanafamilia kwa kwa jina la Yesu.
XXXII. Ninatamka Mafanikio,neema,kuongezeka,kustawi kwenye kila jambo na kwenye kila eneo kwa jina la Yesu
XXXIII. Baraka ya kiagano ya ulinzi wako juu ya familia ikawe juu ya familia yangu kwa jina la Yesu.
Crispin Adam UKUTA WA MAOMBI WhatsApp 0754 56 64 05 AU 0682 94 9191
UKUTA WA MAOMBI-KWA ZOO BUYUNI CHANIKA